Wakala Nami ni mfumo unaowaunganisha Wakala Wakuu na Wakala Wadogo ili kurahisisha usimamizi wa float na ufuatiliaji wa miamala kwa haraka, usalama na ufanisi.

Wakala Mkuu: Ikiwa unataka kusajiliwa na kuanza kutumia huduma zetu, tafadhali wasiliana nasi kwa maelezo zaidi.

Wakala Mdogo: Ikiwa uko tayari kupokea huduma kutoka kwa Wakala Mkuu, pakua programu yetu kupitia Play Store na uanze matumizi mara moja.

Image

Huduma zetu

Wakala nami inakupatia huduma mbali mbali kutokana na shughuli za uwakala. Zikiwemo:

Kuomba na kupokea float

Pata float kwa urahisi na uhakika kutoka kwa mawakala walio kwenye mtandao wako kwa urahisi na haraka.

Usimamizi wa mzunguko wa fedha

Mfumo unaonyesha kwa uwazi fedha zinazoingia na kutoka ili wakala aweze kujua hali yake ya kifedha wakati wote.

Taarifa za miamala

Hifadhi taarifa za miamala na maombi ya float. Fuatilia taarifa kwa urahisi na haraka kwa kupata ripoti ya muda husika.

Ripoti na Takwimu za Kibiashara

Mfumo unatengeneza ripoti mbalimbali za kifedha na utendaji ili kusaidia kufanya maamuzi ya kibiashara.

Taarifa za muda halisi

Mfumo unaonyesha taarifa na mabadiliko yote kwa muda halisi, hivyo maamuzi yanafanyika kwa haraka na kwa usahihi.

Usalama wa taarifa

Kila wakala anahakikiwa na kulindwa kupitia hatua za usalama zinazozuia udanganyifu na matumizi mabaya.

Unataka kuwasiliana nasi?

Tupo hapa kukupa msaada. Wasiliana nasi kwa maswali, maombi ya huduma, au usaidizi wowote unaohitaji.

Faida za Wakala Nami

Wakala nami inakupa faida na kusaidia katila shughuli mbali mbali za mzunguko wa fedha

Loading...