Sera ya Faragha

Kwa kutumia WAKALA NAMI, unakubali sera yetu ya faragha na jinsi tunavyoshughulikia taarifa zako.

Imesasishwa: Desemba 09, 2025

1. Utangulizi

Sera hii ya Faragha ya Makoso Technologies (“sisi”, “kwetu”, au “kampuni”) inaeleza jinsi tunavyokusanya, kutumia, kuhifadhi, na kushiriki taarifa zako unapotumia huduma zetu, ikiwemo programu ya Wakala Nami. Kwa kutumia huduma zetu, unakubali taratibu zilizofafanuliwa katika Sera hii ya Faragha. Ikiwa hukubaliani na sera zetu, tafadhali usitumie huduma zetu.


2. Je, Tunakusanya Taarifa Gani?

Taarifa Unazotupa Kwa Hiari: Tunakusanya taarifa unazojaza wakati wa:

  • Kujisajili katika huduma
  • Kutaka maelezo kuhusu huduma zetu
  • Kutumia huduma ndani ya programu
  • Kuwasiliana nasi moja kwa moja

Aina za taarifa tunazokusanya ni pamoja na:

  • Majina
  • Namba za simu
  • Jina la mtumiaji
  • Neno la siri
  • Njia za mawasiliano
  • Code za watoa huduma
  • Taarifa za eneo
  • Taarifa ya miamala

Data ya Programu: Tunaweza kuomba ruhusa ya kutumia vipengele vya kifaa chako, kama vile:

  • Kamera
  • Namba ya kitambulisho cha kifaa
  • mawasiliano
  • SMS
  • Hifadhi ya kifaa
  • Picha
  • Ruhusa za kutuma taarifa

Unaweza kubadilisha ruksa hizi kupitia mpangilio (Settings) wa kifaa chako.


3. Tunachakataje Taarifa Zako?

Tunachakata taarifa zako kwa madhumuni yafuatayo:

  • Kuwezesha uundaji wa akaunti, kuingia, na kusimamia akaunti yako
  • Kutoa na kuboresha huduma tunazokupatia
  • Kulinda akaunti na mfumo dhidi ya udanganyifu
  • Kuboresha matangazo na maudhui unayoona
  • Kufanya uchambuzi wa ndani ili kuboresha huduma na uzoefu wa watumiaji

4. Tunashirikishaje Taarifa Zako?

Tunaweza kushiriki taarifa zako katika mazingira maalum tu na kwa ufahamu wako, ikiwa pamoja na:

  • Uhamisho wa biashara: Ikiwa kampuni itapata mabadiliko ya umiliki au muundo wa biashara.
  • Washirika wa biashara: Ili kukupa huduma, ofa, au matangazo yanayohusiana.

5. Tunahifadhi Taarifa Zako Kwa Muda Gani?

Taarifa zako zitahifadhiwa kwa muda unaohitajika kutimiza madhumuni yaliyoelezwa katika sera hii. Endapo hakuna haja ya kuendelea kuwa na taarifa zako, tutazifuta au kuzifanya zisiweze kukutambulisha.


6. Tunazilindaje Taarifa Zako?

Tumetumia mbinu za kiusalama za kiufundi na kiutawala kulinda taarifa zako. Hata hivyo, hakuna teknolojia ya mtandaoni iliyo salama kwa 100%, hivyo hatuwezi kutoa uhakika kamili dhidi ya uvamizi wa wahalifu wa kimtandao. Lakini tutajitahitidi kulinda taarifa zako lakini tumia mfumo huu kwenye mazingira salama.


7. Haki Zako za Faragha

Katika baadhi ya maeneo, una haki ya:

  • Kuangalia taarifa zako
  • Kurekebisha taarifa zisizo sahihi
  • Kufuta taarifa zako
  • Kubatilisha ruhusa za kukusanya data

Unaweza kutumia haki zako kwa kuwasiliana nasi:

Barua pepe: wakalanami@gmail.com


8. Vidhibiti vya “Do-Not-Track”

Kwa sasa, hatuwezi kujibu maagizo ya Do-Not-Track (DNT) kutoka kwa vivinjari kwa sababu hakuna taratibu rasmi zilizokubaliwa kimataifa. Tukibadilisha sera hii, tutakujulisha.


9. Mabadiliko ya Sera Ya Faragha

Tunaweza kusasisha Sera hii mara kwa mara. Tarehe ya “Imesasishwa” itaonyesha toleo jipya. Tunashauri usome sera hii mara kwa mara ili kufahamu jinsi tunavyolinda taarifa zako.


10. Mawasiliano

Kwa maswali au maoni, unaweza kuwasiliana nasi kupitia:
Makoso Technologies
Makuburi, Ubungo External,
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: wakalanami@gmail.com


11. Jinsi ya Kuomba Taarifa Zako

Unaweza kuomba ufikie taarifa zako, kuzisasisha, au kuomba zifutwe kwa kutuma ombi rasmi kupitia mawasiliano yetu. Tutalishughulikia kulingana na sheria za ulinzi wa data.

Kusasisha: wakalanami.co.tz/contact

Kufuta: wakalanami.co.tz/delete-account

Loading...